Kenya yaahidi kutenga dola za kimarekani bilioni 8 kupambana na mabadiliko ya tabia nchi katika miaka kumi ijayo
2021-04-23 09:43:33| cri

 

 

Katibu mkuu wa wizara ya mazingira na misitu ya Kenya Bw. Chris Kiptoo, amesema Kenya itatoa dola za kimarekani bilioni 8 kupambana na mabadiliko ya tabia nchi katika miaka kumi ijayo.

Bw. Kiptoo amesema hii ni ahadi ya Kenya, na Kenya imetambua kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni jambo la kweli, na Kenya lazima iweke raslimali yake yenyewe kukabliana na suala hilo.

Vilevile amesema ingawa Kenya ni mchangiaji mdogo kwa uzalishaji wa hewa ya ukaa, lakini inakabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya taiba nchi.