Nchi zilizoendelea zatakiwa kuheshimu ahadi ya msaada wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
2021-04-23 19:30:08| CRI

 

 

Nchi zilizoendelea zimetakiwa kuheshimu ahadi yao ya kutoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akiongea jana kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika kwa njia ya video, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, amesema ni lazima nchi zilizoendelea zitoe fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwa ni pamoja na dola za kimarekani bilioni 100 zilizoahidiwa kwa ajili ya mpango wa utekelezaji kwa nchi zinazoendelea, kwenye mkutano wa kundi la G7 uliofanyika Juni 7. 

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini pia ametoa mwito kwa nchi zilizoendelea kutoa msaada huo, lakini isiwe sehemu ya msaada wa kawaida wa maendeleo. Amesema kama msaada huo ukiwa kwenye mtindo wa mkopo, mzigo wa madeni kwa nchi zinazoendelea unakuwa mkubwa.