Wanablogi wengi wanaonesha utajiri wao kwa video fupi
2021-04-28 18:22:13| Cri

“Ni uzoefu wa namna gani kukaa katika chumba cha rais kwenye hoteli kinachogharimu dola za kimarekani 11,511 kwa usiku mmoja?” Video mbalimbali zinazoonesha utajiri kama hii zimekuwa zinaonekana kwenye majukwaa ya video fupi nchini China.

Hivi karibuni wanablogi kadhaa ambao wanajulikana kwa kuonesha mitindo ya maisha ya utajiri walifuta video kama hizo na kuomba msamaha kwa kuleta athari mbaya kwa jamii. Msamaha huo ulikuja baada ya baadhi ya wanamtandao kuwakosoa. Kutengeneza video zinazoonesha utajiri kunaenea sana kati ya wanablogi, kwani kunavutia mashabiki wengi huku zikigharamu pesa ndogo.

Wengi kati ya wanablogi kama hao wenyewe sio matajiri, lakini wana timu ambayo ina uhusiano na idara za kushughlikia bidhaa zenye thamani kubwa. Mwanablogi mmoja alipata mashabiki milioni 22 kwenye jukwaa la video fupi ndani ya miaka mitatu kwa kupiga video kama hizo.

Baadhi ya wanamtandao wa China wanaona video hizi si mbaya, kwani maisha ya matajiri yapo, na watu haki ya kujua hali kama hizo. Lakini wengi wana maoni tofauti wakiona kuwa, kila mwanablogi mwenye idadi kubwa ya mashabiki, anapaswa kutambua kuwa akiwa mtu anayejulikana, anahitaji kuwa na wajibu wa kijamii katika kueneza maadili mema. Lakini wengi wao wanakosa ufahamu huu na kuangalia tu kupata mapato kama lengo lao.