Shanghai: Mayaya au walezi wa watoto watakiwa kupewa mafunzo ya lugha
2021-05-06 10:30:51| Cri

Mji wa Shanghai hivi karibuni umetoa mwongozo wa kuimarisha kazi za lugha katika zama mpya, kifungu kimoja kimetaka mayaya au walezi wa watoto, walimu na watumishi wa serikali wapewe kipaumbele katika mafunzo ya lugha sanifu ya taifa yaani Mandarin.

Imefahamika kuwa kutokana na juhudi za kizazi baada ya kizazi, maendeleo makubwa yamepatikana kwenye kazi ya mafunzo ya lugha mjini Shanghai, na asilimia 90 ya wakazi wanaweza kuongea Mandarin, kiwango ambacho ni asilimia 5 juu ya lengo la taifa la mwaka 2025. Serikali ya Shanghai imeamua kuwa katika hatua ijayo, mji huo utaanza operesheni tano maalumu ili kuimarisha zaidi maendeleo yaliyopatikana.

Mwongozo huo pia unasisitiza kuwa inapaswa kuimarisha ujenzi wa maadili ya lugha, na kuzuia ukatili wa kilugha na kuenea kwa lugha chafu, haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, SHANGHAI pia itaimarisha ujenzi wa mazingira yasiyo na vizuizi kwa watu wenye ulemavu wa kuona na kusikia, na kutoa huduma ya utafsiri ya lugha ya ishara wakati serikali inapotangaza habari muhimu au habari zinazohusiana na maisha ya watu.