RIADHA: Waandaaji wa riadha ya dunia U-20 wapokea awamu ya kwanza ya vifaa
2021-05-13 15:56:31| cri

Kamati ya Ndani ya Maandalizi ya Mashindano ya Riadha ya Dunia Chini ya Miaka 20 (U-20) nchini Kenya (LOC) imepokea awamu ya kwanza ya vifaa vya michezo kwa maofisa na watu watakaojitolea katika mashindano hayo ya dunia kwa vijana yaliyopangwa kufanyika kuanzia Agosti 17 hadi 22 katika viwanja vya Kasarani. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jack Tuwei amepokea vifaa hivyo vilivyotolewa na wadhamini wa mashindano ya riadha duniani Asics katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Moi. Amesema bado wanasubiri vifaa vingine zaidi kwa ajili ya mafundi, mazoezi na vya mashindano kutoka kwa wasambazaji walioidhinishwa na Shirikisho la Riadha Duniani, ambavyo vinatarajiwa kufika nchini Kenya mwezi Julai.