Wazazi wawataka watoto kuuza vitu katika soko la usiku
2021-05-14 10:34:15| Cri

Jiang Jiali na mkewe kutoka Mji wa Lanzhou wote ni waigizaji wa Opera na mapato ya familia yao ni RMB yuan laki tano, sawa na dola za kimarekani elfu 78. Waliwafanya binti yao mwenye umri wa miaka 11 na  mdogo wao wa kiume kuuza vitu katika soko la usiku. Wanawataka watoto watafute njia ya kuwavutia wateja. Kibanda chao kinafungwa saa nne na nusu usiku, na baba Jiang Jiali alikuwa akiwaangalia kwa siri kutoka mbali.

Baba alisema kuwa lengo la kitendo hicho ni kuwafanya watoto wapate uzoefu katika jamii, na wasiwe na tabia mbaya kutokana na ukosefu wa fedha. Alisema watoto walishughulikia bidhaa zote wanazouza, na ubao wa duka lao pia ulibuniwa na kutengenezwa na watoto wenyewe. Binti wao alisema, ikilinganishwa kuendesha duka, kusoma shule ni jambo rahisi zaidi, na anataka kusoma kwa bidii zaidi katika siku zijazo.