Chama cha uzalishaji Uganda chakata kuondolewa kwa ushuru wa stampu ya kidijitali
2021-05-14 17:08:00| cri

Kampuni za vinywaji nchini Uganda kupitia chama cha uzalishaji nchini humo imeitaka serikali ya Uganda kubeba mzigo wa kutekeleza kodi ya  ushuru wa kidijitali ulioanzishwa mwaka was 1919 na 2020 kuisaidia serikali kufuatilia zoezi la ulipaji ushuru .  Chama hicho kimesema hatua hiyo kitasaidia kudhibiti gharama ya uzalishaji  hasa wakati huu ambapo janga la corona limeathiri biashara kwa kiwango kikubwa.  Hatua hiyo, wameongeza kuwa itawalinda wawekezaji wa sekta hiyo ambao hivi sasa uzalishaji wao umepungua kwa asilimia 40 huku soko likiwa limepungua kwa asilimia 65. Hivi sasa janga la corona limeendelea kuathiri sekta ya uzalishaji nchini humo na kusababaisha watu wengi kupoteza ajira. Chama hicho kimesema uwezo wao wa uzalishaji umepungua kwa asilimia 40 huku wakiendelea kulipa ushuru wa stampu kwa njia ya kidijitali. Novemba mwaka juzi, Mamlaka ya kodi nchini Uganda ilitangaza kuzindua ushuru wa stampu kwa njia ya kidijitali kwa uzalishaji wa bidhaa nchini humo