SOKA: Hatma ya Ronald Koeman ndani ya Barcelona mashakani
2021-05-14 17:00:07| cri

Klabu ya FC Barcelona imewasiliana na Kocha wa Klabu ya Bayern Munich, Hansi Flick ili kuja kufundisha timu hiyo msimu ujao na hivyo kuzua mashaka mustakabali wa Ronald Koeman. Mwezi uliopita, Flick aliweka wazi nia yake ya kuachana na Bayern mwishoni mwa msimu, lakini ilielezwa kuwa alikuwa akikaribia kuchukua nafasi ya Joachim Low kama Kocha wa Ujeruman. Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman amesaliwa na mwaka mmoja katika kandarasi yake ndani ya Camp Nou lakini imeripotiwa kuwa kuna sitofahamu ndani ya bodi ya klabu hiyo juu ya maamuzi ya hatma ya baadaye ya Koeman.