Tanzania yataka kuongezwa katika uwekezaji wa mifugo na mbegu za malisho
2021-05-14 17:06:10| cri

Serikali ya Tanzania imetaka kuongezwa kwa uwekezaji wa mifugo na mbegu za malisho kwa kipindi cha mwaka mzima.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania Bw Elisante Ole Gabriel alisema hayo wakati akifungua warsha maalum ya wadau wa uzalishaji wa mbegu za malisho ili kijadili namna kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo nchini humo. Amesema kuwa takwimu zinaonesha  kiwango cha uzalishaji wa mbegu ni mdogo ukilinganisha na mahitaji yake na kwamba kama wawekezaji watageuza changamoto hiyo kuwa fursa itasadia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji. Aidha amesema serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo na makampuni na watu binafsi wenye nia ya kuzalisha mbegu bora za malisho, kufanya kazi hiyo kibiashara kwa kuwapa mwongozo unaostahili.

Amebainisha kuwa lengo ni kufanikisha juhudi za serikali hasa kujiletea faida za kiuchumi kupitia uwepo wa fursa ya wingi wa mifugo nchini humo na hata kuuza malisho katika mataifa mengine