Bunge la Afrika Kusini lajadili waraka kuhusu ndoa ya mke mmoja waume wawili
2021-05-21 13:52:57| Cri

Mwishoni mwa mwaka jana kwenye mjadala mmoja kuhusu changamoto za kukosekana kwa idadi ya watu hapa China, Profesa Youguang Huang wa Chuo Kikuu cha Fudan cha Shanghai alisema changamoto ya kukosekana kwa uwiano kwenye idadi kati ya wanaume na wanawake inahitaji, sheria za nchi zibadilishwe ili mwanamke aweze kuolewa na wanaume wawili. Profesa huyo alisema tatizo la kukosekana kwa uwiano wa idadi ya wanawake na wanaume, (yaani wanaume kuwa wengi kuliko wanawake) litaongezeka na halitapungua. Hii ni kutokana na kuwa mwelekeo wa hali ya uzazi ya China haonyeshi kuwa idadi ya watu itaongezeka sana, na hata kama ikiongezeka hali ya watu kupendelea kuwa na mtoto wa kiume kama ilivyo sasa, ina maana idadi watoto wa kiume itazidi kuwa kubwa. Profesa alisema baada ya miaka mitano hadi kumi, idadi ya wanawake wasio na ndoa wenye umri wa kuolewa haitaongezeka, na ya wanaume wanaotoka kuona itaongezeka. Hali hii italeta urahisi sana kwa wanawake wanaotaka kuolewa, lakini itakuwa taabu na ushindani mkali kwa wanaume kupata jiko. Profesa alisema katika mazingira kama haya, mahitaji ya kimwili na kisaikolojia kwa wanaume wasio na wake hayawezi kutoshelezwa vizuri, na hii utakuwa hatari. Hoja ya mke mmoja waume wawili ya Profesa huyo, ilijikita kukabiliana na changamoto ya wanaume kukosa wake, na kuepusha hatari inayoweza kutokea baadaye kutokana na wanaume kugombea wanawake. Hoja hili ilikosolewa vikali kwa kuwa ni kinyume kabisa na maadili ya jadi ya wachina, na ukosoaji ulitoka karibu kila kina ya nchi.

Lakini hivi karibuni hoja kama hii imeingia kwenye bunge la Afrika Kusini, baada ya waraka mmoja kufikishwa bungeni kujadili suala hilo. Tofauti na hapa China ambapo suala ni kukosekana kwa uwiano kwenye idadi ya wanaume na wanawake, yaani wanaume kuwa wengi kuliko wanawake, nchini Afrika Kusini hoja ilikuwa ni usawa. Baadhi ya wabunge waliojadili hoja hiyo, walihoji kwanini sheria hazizuii mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini zinazuia mwanamke kuwa na mume zaidi ya mmoja. Kulikuwa na mjadala mkali ambao kimsingi haukipatiwa majibu, na mpaka sasa mjadala unaendelea.