Manchester City yaizawadia Everton 5G na kuondoka na kombe
2021-05-24 18:18:34| cri

Msimu wa Ligi Kuu England ulikamika jana Mei 23 kwa mabingwa wapya, Manchester City wanaonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola kutwaa ubingwa huo kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Everton, Uwanja wa Etihad. Ni Kevin De Bruyne alipachika bao dakika ya 11, Gabriel Jesus dakika ya 14, Phil Foden dakika ya 53 na nyota wao Sergio Aguero alipachika mabao mawili dakika ya 71 na 76. Timu ya Liverpool nayo ambayo ilikuwa haipewi nafasi ya kumaliza ndani ya tano bora, ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace umewafanya wamalize wakiwa nafasi ya tatu na pointi 69, na Chelsea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa wanauhakika wa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa inamaliza ikiwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 67. Nne bora kwa msimu wa 2020/21, Manchester City ni namba moja wakiwa na pointi 86, namba mbili ni Man Chester United ambao wao walishinda mabao 2-1 dhidi ya Wolves namba tatu ni Liverpool, nne ni Chelsea na tano ni West Ham United ikiwa na pointi 65.