NDONDI: Manny Pacquiao kuonekana tena ulingoni baada ya miaka miwili
2021-05-24 18:17:53| cri

Manny Pacquiao anatarajiwa kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili atakapokuwa akipigana na bingwa wa WBC na IBF uzito wa kati Error Spence mwezi August mwaka huu. Pacquiao mwenye umri wa miaka 42, hajapigana pambano lolote tangu amchakaze Keith Therman alipokuwa akiwania ubingwa wa WBA uzito wa kati mnamo mwezi Julai mwaka 2019. Kwenye ukurasa wake wa Twitter Pacquiao amethibitisha atapanda ulingoni dhidi ya Spence mwenye umri wa miaka 31. Pambano hilo litakuwa ni la 72 kwa Pacquiao ambapo ameshinda 62, kapoteza 7 na sare 2 katika rekodi zake na anawania ubingwa wa Dunia katika muongo wa nne tangu atwae wa kwanza mwaka 1998 .