SOKA: Mwenyekiti wa klabu ya PSG Al-Khelaifi afunguka juu ya hatma ya Mbappe PSG
2021-05-25 18:24:02| cri

Mwenyekiti wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi amesema anaimani kubwa kuwa mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappe atasalia klabuni hapo licha ya kuwepo kwa fununu kuwa nyota huyo ananukia Real Madrid ya Hispania. Akizungumza baada ya mchezo wa mwisho wakutamatisha ligi kuu ya Ufaransa ambao PSG waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuukosa ubingwa wa Ufaransa, Khelaifi alisema Kylian ni mchezaji wa PSG, na ataendelea kuwa mchezaji wa PSG. Mbappe ni mfaransa na ni mtu halisi wa PSG badi ana mkataba nao na anataka kusalia kwa 100%".  Baada ya kusema hayo, Mbappe mwenyewe akafunguka kuhusu vitu anavyotaka viwepo PSG ili kumfanya asalie klabuni hapo ikiwemo kuona kuna mipango ya mafanikio. Mbappe aliyasema hayo baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Ufaransa na mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kufunga mabao 27 na kuchukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo.