NBA: Hatua ya Mtoano yaendelea kwa kasi Marekani
2021-05-25 18:23:24| cri

Michezo ya mtoano ya kutafuta timu nne zitakazocheza hatua ya nusu fainali kwa timu kutoka pande zote za Mashariki na Magharibi mwa NBA 'Playoffs' imeendelea kushika kasi alfajiri ya kuamkia jana kwa michezo miwili, Atlanta Hawks ikipata ushindi wa alama 107 kwa 106 dhidi ya New York Knicks. Trae Young wa Atlanta ameibuka kuwa nyota wa mchezo huo kwa kupata alama 32, rebaundi 7 na assisti 10 huku Memphis Glizzlies wakipata ushindi wa alama 112-109 dhidi ya Utah Jazz wakati ambapo nyota wake Dillon Brooks ameibuka kidedea kwa kufikisha alama 31, rebaundi 7 na Assisti 2. Michezo ya NBA playoff kwa mzunguko wa kwanza imeendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo miwili ambapo Miami Heats imepambana na Milwaukee Bucks huku Denver Nuggets ikivaana na Portland Trail Blazers.