SOKA: Clatous Chama mtaalamu wa mabao ya lala alama aweka rekodi kimataifa
2021-05-25 18:23:40| cri

Nyota wa wawakilishi wa Tanzania, Simba Clatous Chama ameweka rekodi katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutinga hatua ya nusu fainali. Nyota huyo ambaye amekuwa bora ndani ya Simba anashikilia rekodi ya kuwa mtaalamu wa kufunga mabao ya dakika za lala salama pale anapopata nafasi ya kufunga Uwanja wa Mkapa. Ukiacha mbali rekodi yake ya Mei 22, Uwanja wa Mkapa Simba ilipoibamiza Kaizer Chiefs 3-1 wakati Chama alipopachika bao dakika ya 86 kwa pasi ya mshikaji wake Luis Miquissone ana mabao mengine aliyapachika nyuma dakika za lala salama kwenye ligi za mabingwa Afrika namna hii, Machi 16, 2019, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-1 AS Vita ilikuwa ni hatua ya makundi, Chama alipachika bao dakika ya 89. Disemba 23, 2018 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-1 Nkana, Chama alipachika bao la mwisho na la ushindi dakika ya 90. Novemba 28,2018, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 4-1 Mbabane Swallows, Chama alipachika bao la lala salama dakika ya 90+1 ilikuwa ni hatua ya awali.