Lakers kuvaana na Phoenix Suns NBA Playoff
2021-05-26 18:20:23| cri

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya kikapu nchini Marekani 'NBA', timu ya Los Angeles Lakers imeibua hofu ya kutetea taji hilo baada ya kukubali kufungwa usiku wa kuamkia jana na Phoenix Suns kwa alama 99 kwa 90 ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kwenye NBA Playoff. Lakers wanahitaji kushinda michezo minne kati ya mitano iliyosalia kwenye hatua hiyo ya mtoano ili kutinga hatua ya nusu fainali ya NBA kwa upande wa Mashariki mwa ligi hiyo ambayo mpaka hivi sasa vinara wa upande huo Philadelphia 76ers wakionekana kufanya vizuri. Michezo ya mtoano ya NBA imeendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo mitatu huku Lakers wakishuka tena na Phoenix Suns, Brooklyn Nets itakipiga tena na Boston Celtics.