BASKETBALL: Davis, Lebron na Durrant hawakamatiki NBA Playoff
2021-05-27 17:09:22| cri

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA', Los Angeles Lakers imeibuka na ushindi wa kwanza kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa hatua ya mtoano ya robo fainali ya ligi hiyo iliyochezwa jana dhidi ya Phoeniz Suns. Kwenye mchezo huo uliokuwa wakukata na shoka, nyota wawili wa Lakers, Lebron James na Anthony Davis ndiyo walioonesha utofauti mkubwa wa ubora mbele ya Suns, kwani Davis ameibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kupata alama 234rebaundi 10 na assisti 7. Lebron James amepata alama 23, rebaundi 4 na assisti 9 huku nyota wa Suns David Booker akiwa kinara kwa upande wa timu yake kwa kufikisha alama 31, rebaundi 1 na Assisti 3.