SOKA: Gomes ampotezea wakala wa Kagere
2021-05-27 17:09:04| cri

Kocha mkuu wa Simba SC Didier Gomed da Rosa amesema hana muda wa kujibu tuhuma alizorushiwa na wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere. Patrick Gakumba, wakala wa mshambuliaji huyo alimtuhumu Gomes, baada ya Meddie Kagere kushindwa kutumika wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs. Gakumba, alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kwao Rwanda na Tanzania, akisema kutolewa kwa Simba kwenye michuano ya Afrika kumechangiwa na kocha Gomes kwa kushindwa kumtumia Kagere.