RIADHA: Selous Marathon kufanyika Agosti 21 Morogoro
2021-05-28 15:38:50| cri

Shindano la riadha la Selous Marathon linalotarajia kufanyika Agosti 21, mwaka huu katika mkoa wa Morogoro nchini Tanzania, limepewa jina la Kijani Project. Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Shindano hilo Imani Kajula, amesema kuwa mwaka huu itakuwa ya kitofauti kwa kuwa inafanyika mkoani Morogoro, na kuwahakikishia ulinzi wa kutosha washiriki wote wa mbio hizo pamoja na kuwalipia bima ya maisha. Amesema katika mbio hizo, washiriki watapata medali, na kutakuwa na medali tofauti kilamwaka zitakazotambulisha mshiriki popote.