SOKA: Barcelona kupitisha fagio la chuma
2021-05-28 15:39:36| cri

Rais wa Barcelona, Joan Laporta yupo tayari kupitisha panga kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Nou Camp kusafisha wachezaji wasiohitajika na kuleta wengine wapya kupiga kazi. Antoine Griezmann na Philippe Coutinho ni miongoni mwa mastaa ambao huenda watakuwa kwenye orodha hiyo ya watakaopigwa bei dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Wachezaji wengine wanaotajwa huenda wakaondoka ni Ousmane Dembele, Miralem Pjanic, Martin Braithwaite, Junior Firpo na Neto. Wachezaji ambao hawataguswa kabisa ni Lionel Messi, Frenkie de Jong, Marc-Andre ter Stegen, Ronald Araujo, Oscar Mingueza, Pedri, Ilaix Moriba na Ansu Fati.