WAVU: Mashindano ya Wavu yashika kasi
2021-05-28 15:39:56| cri

Mashindano ya Mpira wa Wavu yameendelea kutimua vumbi katika Uwanja wa Chuo cha Mafunzi kisiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu ya Nyuki na Mafunzo. Katika mchezo huo, timu ya Mafunzo ilitawala mchezho huo na kuibuka na ushindi wa seti 3 – 0. Nahodha wa timu hiyo Yusuph Mussa amesema, timu yake itazidi kuongeza juhudi na kushinda michezo iliyobakia ili kunyakua ubingwa wa Ligi hiyo. Naye nahodha wa Nyuki Ayubu Abasi amesema, sababu ya kupoteza mechi hiyo ni kutokuwa na uwanja wa mazoiezi na hivyo kulazimika kufanya mazoezi kwenye viwanja visivyokuwa na vifaa muhimu kwa ajili ya mchezo huo.