China yatoa waraka kuhusu mfumo wake wa chama cha kisiasa
2021-06-25 11:03:44| cri

China yatoa waraka kuhusu mfumo wake wa chama cha kisiasa_fororder_999

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka uitwao “Mfumo wa Chama cha Kisiasa wa China: Ushirikiano na Mashauriano”, ukielezea sifa maalum na nguvu ya mfumo wa chama cha kisiasa wa nchi hiyo.

Waraka huo umesema, mfumo wa aina mpya wa chama cha kisiasa wa China unajumuisha Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama vinane vya demokrasia pamoja na watu wasio na chama chochote. Kwa muda mrefu, CPC imekuwa ikishirikiana na vyama mbalimbali vya demokrasia, kujitahidi kwa pamoja, kusonga mbele kwa pamoja, kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kujenga uhusiano wa karibu wa ushirikiano.

Waraka huo umesema, mfumo huo unashikilia moyo wa ushirikiano, ushiriki na mashauriano, umoja, demokrasia na masikilizano, na unatoa nafasi kwa ushirikiano wa kisiasa, kudai maslahi, kushirikisha rasilimali kwenye jamii, usimamizi wa kidemokrasia na ulinzi wa utulivu. Pia kutimiza uhusiano mzuri wa kutawala kisiasa na kushiriki kisiasa, kuongoza na kushirikiana, kushauriana na kusimamia, na kuongeza kuwa, muundo huo ni muhimu kuwawezesha wananchi wawe wenyeji wa nchi na mfumo wa demokrasia ya kushauriana katika mfumo wa ujamaa.

Waraka umesisitiza kuwa katika utawala wa nchi, CPC, vyama vya demokrasia na watu wasio na chama chochote wanashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja, na huu ni mpango muhimu wa kimfumo katika mfumo wa chama cha kisiasa cha China wa aina mpya, ambao umeanzishwa kwa kufuata mkondo wa historia, kwa ubunifu, na una sifa nzuri na nguvu kubwa ya uhai.

Mfumo huo unaolingana na hali halisi ya China na mahitaji ya usimamizi wa nchi unasaidia kuhuisha nchi, kuendeleza jamii na kuboresha maisha ya watu.