Rais Xi Jinping wa China atoa hutuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC
2021-07-01 12:18:21| cri

Rais Xi Jinping wa China atoa hutuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC_fororder_QQ图片20210701121701

Mkutano mkuu wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) leo umefanyika hapa Beijing.  Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo.

Kwenye hotuba yake, rais Xi ametanga kuwa China imetimiza lengo la kwanza la karne, yaani kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

Amesema hii inamaanisha kuwa China imetatua tatizo la umaskini uliokithiri nchini China na inaelekea kutimiza lengo la pili la karne la kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa yenye nguvu katika pande zote. Amesisitiza kuwa China imepita vipindi vya kujikomboa, kutajirika na kuwa na nguvu kubwa, na sasa mchakato wa ustawi tena wa taifa la China haupinduki.

Amesema maendeleo ya China yatatoa fursa kwa dunia nzima, na China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kukuza ujenzi wa uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kusukuma mbele maendeleo yenye kiwango cha juu ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Pia amesisitiza kuwa, China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa dunia, na Chama cha Kikomunisti cha China kitashikilia kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupinga umwamba.

Rais Xi amesema uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa, kwani uongozi wa Chama hicho ni sifa ya kimsingi ya Ujamaa wenye Umaalum wa China na kutoa nguvu kubwa kwa mfumo huo. Ameongeza kuwa uongozi wa CPC ni msingi na damu ya Chama na nchi, na una uhusiano wa karibu na maslahi na mustakbali wa watu wote wa China.

Amesema daima CPC kinawakilisha maslahi ya kimsingi ya wananchi, na kuishi kwa kutegemeana na wananchi, na hakina maslahi yoyote maalum, na kamwe hakiwakilishi maslahi ya kundi lolote lenye mamlaka, na watu wenye hadhi maalum. Ameongeza kuwa, jaribio lolote la kutenganisha chama hicho na watu wa China kwamwe halitafanikiwa. Pia amesisitiza kuwa, CPC lazima kizingatie madhumuni ya kimsingi ya kuwahudumia wananchi kwa moyo wote, kufuata msimamo wa wananchi, na kuhimiza mchakato wa maendeleo ya pande zote ya binadamu, pia kuhakikisha wananchi wote wanapata maendeleo makubwa zaidi na kutajirika kwa pamoja.

Aidha, rais Xi amesema kamwe Wachina hawataruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuwaonea, kuwakandamiza au kuwatweza, na mtu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakumbana na ukuta mkubwa wa chuma uliojengwa na watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China. Amesema China haijawahi kuonea, kudhulumu, au kuwatisha watu wa nchi nyingine yoyote, na kamwe haitafanya hivyo. Amesema siku zote China imekuwa ikifanya kazi ya kulinda amani ya ulimwengu, kuchangia maendeleo ya dunia, na kulinda utulivu wa kimataifa, na ametoa mwito wa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

Xi Jinping: Uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa

Rais Xi Jinping wa China atoa hutuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC_fororder_QQ图片20210701121708