Mkutano wa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika leo Julai Mosi katika Uwanja wa Tian’anmen mjini Beijing. Katibu mkuu wa Kamati kuu ya CPC, rais wa China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya CPC Xi Jinping amehudhuria na kuhutubia mkutano huo.
Wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya kidemokrasia, Shirikisho la viwanda na biashara la China na wazalendo wasio wanachama wa chama chochote wametoa pongezi kwa pamoja. Watu zaidi ya elfu sabini wameshiriki kwenye mkutano huo.