Tanzania yakamata kilo 99.33 za dawa za kulevya katika mwezi Juni
2021-07-20 08:54:50| CRI

Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ya Tanzania imesema imekamata kilo 99.33 za dawa za kulevya mwezi Juni mjini Dar es Salaam na kuwakamata watuhumiwa nane.

Kamishna mkuu wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Bw. Gerald Kusaya, amesema watuhumiwa hao ni pamoja na afisa wa polisi, maafisa wawili na mamlaka ya kodi ya Tanzania na wafanyabiashara watano.

Dawa hizo haswa heroin na methamphetamine zilikamatwa katika operesheni maalum ya ushirikiano iliyofanywa na DCEA, polisi na Mamlaka ya kodi ya Tanzania.