East Africa: Djibouti, Ethiopia kuzindua Kiunga cha Pili cha umeme
2021-07-21 07:45:36| CRI

Djibouti na Ethiopia wamepata fedha za kujenga njia ya pili ya kusafirisha umeme baada ya majirani hao wawili kufurahiya mapato kutoka kwa mradi wa kwanza ambao uliunganisha gridi zao za umeme.

Mradi wa kwanza umeiwezesha Djibouti kuagiza umeme, mbadala na nafuu wa Ethiopia.

Baada ya, nchi hizo mbili kukubadili kuendeleza mradi huo, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) sasa imeidhinisha mikopo miwili ya ruzuku yenye thamani ya $ 83.6 milioni ambayo inaiwezesha Ethiopia na Djibouti kuendelea na ujenzi wa njia yao ya pili ya kusafirisha umeme ambayo mwishowe itaongeza biashara ya Nishati.

Kulingana na taarifa kutoka kwa benki, Bodi ya Wakurugenzi ya Kikundi cha Benki ya Maendeleo ya Afrika iliidhinisha fedha hizo kwa lengo la kukuza biashara ya umeme wa mpakani kati ya Ethiopia na Djibouti.

Misaada hiyo pia inakusudia kuimarisha ujumuishaji wa uchumi katika sehemu ya Afrika Mashariki.

Fedha hizo zinajumuisha ruzuku ya dola milioni 69.65 kwa Ethiopia na ruzuku ya pili ya $ 13.93 milioni kwa Djibouti.