Waziri wa mambo ya nje wa China asema ziara yake katika Mashariki ya Kati inalenga kukuza urafiki na ushirikiano
2021-07-22 08:59:32| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi amesema lengo la ziara yake nchini Syria, Misri na Algeria ni kusukuma mbele utekelezaji wa mwafaka uliofikiwa kati ya Rais Xi Jinping wa China na wakuu wa nchi hizo tatu, na kuimarisha urafiki.

Bw. Wang alisema hayo alipokutana na wanahabari wa China baada ya kukamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati.

Alisema ziara yake pia inalenga kuongeza hali ya kuaminiana, kuimarisha ushirikiano, kuhimiza amani na utulivu wa kikanda, kusukuma mbele umoja na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, na kulinda haki na usawa wa kimataifa.

Bw. Wang Yi amesema yeye na wenzake wa nchi hizo tatu wamekubaliana kuongeza mawasiliano na uratibu wa kimkakati, kuendelea kuungana mkono kwenye masuala yanayohusisha maslahi makuu na ufuatiliaji mkubwa wa kila upande, na kutoa michango mipya katika ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na nchi za Kiarabu.