Akina Mama Washauriwe Kuchangia Uchumi Dijitali
2021-07-22 08:04:50| CRI

RIPOTI ya hivi majuzi kuhusu matumizi ya intaneti miongoni mwa wanawake barani Afrika inashtua kwani wanawake wengi sana bado wameachwa nje katika uchumi wa dijitali.

Katika takwimu zilizotolewa na shirika la GSMA kwenye ripoti ya Pengo la Matumizi ya Simu Kijinsia, zaidia ya wanawake milioni 74 hapa barani bado hawajajiunga na mitandao ya intaneti wala kumiliki simu.

Ikilinganishwa na wanaume, kuna pengo la wanawake wapatao milioni 234 katika matumizi ya intaneti kuboresha shughuli za kila siku.

Hii inamaanisha kuwa tunazungumzia kuhusu ajira katika uchumi wa kisasa, mamilioni ya wanawake barani hawana uwezo wa kupata fedha wanazopata wanaume, hali ambayo inawadidimisha zaidi wanawake, kando na taasubi zilizopo za kitamaduni.

Tatizo la wanawake kusalia nyuma wanaume wakipiga hatua kwenye biashara za kidijitali linafaa kutatuliwa na wanawake wenyewe.