Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani kufanya ziara nchini China
2021-07-22 09:45:35| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Wendy Sherman Julai 25 na 26 atafanya ziara mjini Tianjin, China.

Msemaji huyo amesema, Marekani imependekeza kupanga Bi. Sherman kufanya ziara nchini China kubadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya pande mbili. Baada ya pande mbili kukubaliana, Bi. Sherman atafanya ziara huko Tianjin Julai 25 na 26.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, naibu waziri wa mambo ya nje wa China anayeshughulikia uhusiano kati ya China na Marekani Bw. Xie Feng, atafanya mazungumzo na Bi. Sherman, na baadaye waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi pia atakutana na Bi. Sherman.