Uganda: URA yaokoa shilingi bilioni 651.7 kutoka kortini na kukamata bidhaa
2021-07-27 07:45:45| cri

Mamlaka ya ukusanyaji ushur nchini Uganda URA,  imeokoa jumla ya shilingi bilioni 651.7 kwa mwaka wa ferdha wa 2020/2021. Juhudi hizi zimetokana na mikakati ya upepelezi wa ulipaji ushuru, masharti makali kwa wanaokwepa kulipa ushuru, kukamata mali ya magendo, miongoni mwa hatua zingine. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya URA ya kila mwaka iliyowasilishwa kwa waandishi wa habari na kamishena jenerali  wa Mamlaka hayo, Bwana John Musinguzi.

Shilingi hizi bilioni 651.7 zilichangai asilimia 14 ya jumla ya mapato yote yaliyokusanywa na URA mwaka wa fedha wa 2020/21. Hii ni licha ya kuwa URA ilifunga mwaka huo wa kifedha ikiwa na pengo la shilingi trilioni 2.3 katika makusanyo yake ya kila mwaka.