Afrika: Kampunzi ya Sameer Afrika yawaachisha kazi waajiriwa 107
2021-07-27 07:44:38| cri

Kampuni ya kutengeneza magurudumu ya magari, Sameer Afrika, inaonekana kuyumbishwa sana kiuchumi, baada ya kupunguza wafanyikazi wake. Kampuni hii ya kutengeneza na kusambaza magurudumu barani Afrika, imekuwa ikipitia wakati mgumu haswa kifedha kwa miaka kadhaa iliyopita.

Kwenye ripoti yake ya kila mwaka ya 2020, Sameer Africa ilisema kwamba imelazimika kuwaachisha kazi watu 107, na vile vile, kuuza mali yake yenye thamani isiyojulikana ili kujikwamua kifedha.

Kati ya wale waliochishwa kazi ni wasimamizi wapatao 75. Kwa jumla Sameer imeokoa zaidi ya dola milioni 2.28 baada ya kuwaachisha kazi wajiiriwa wake 107.