Tanzania: Wanafunzi wa kilimo waomba serikali kuwapunguzia gharama wakulima
2021-07-27 07:45:23| cri

Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Chuo Kikuu cha Kilimo xha China (CAU), wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwapunguzia gharama ya uzalishaji wakulima ili kuendana na kipato chao. Chuo hicho kinatekelza mradi wa pamoja wa kupunguza umaskini kwa wakulima wadogo mkoani morogoro.

Wanafunzi hao wanaosoma kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya usafiri iliyosababishwa na ugonjwa wa corona, walitoa rai hiyo juzi, baada ya kufanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vinavyotekelza mradi huo mkoani Morogoro.

Ziara hiyo ililenga kuangalia namna chuo hicho kinavyotekeleza miradi mbalimbali hasa ya kilimo cha mahindi katika kusaidia kuwapunguzia wakulima umaskini kwa utoaji mafunzo ya uzalishaji wa mazao kwa tija.