Waziri Mkuu wa China Li Keqiang asisitiza juhudi zote za kudhibiti mafuriko na misaada baada ya maafa
2021-07-27 10:42:05| Cri

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang ametoa wito juhudi zote za kudhibiti mafuriko na kutoa misaada ya majanga, na kutoa kipaumbele usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Mvua zimesababisha hasara kubwa na vifo vya watu katika baadhi ya maeneo ya China. Bw. Li ametoa wito kuchukua hatua kamili za usalama za kupunguza hasara ili kukabiliana na mvua kubwa na kimbunga kilichotabiriwa kutokea katika maeneo ya pwani, kaskazini mwa China. Ametaka juhudi za kutuma timu na vifaa vya kitaalam kwa wakati na kutoa habari wazi za uokoaji.

Aidha ameagiza kuimarisha utaratibu wa kudhibiti majanga ili kuboresha uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura nchini na ufahamu wa watu juu ya kujilinda.