Usafirishaji wa bidhaa kuboreshwa Uganda
2021-08-16 07:37:01| cri

Usafirishaji wa bidhaa kutoka eneo la viwandani la Namanye nchini Uganda unatarajiwa kuboreshwa baada ya wazalishaji wengi katika eneo hilo kulalamikia gharama ya uzalishabi bidhaa katika eneo hilo.Wamiliki wa viwanda katika eneo hilo wamesema wakati mwingi walazimika kukodi malori mengi kwa ajili ya kusafirisha bidhaa zao kwa wateja kutokana na barabara mbovu katika eneo hilo.Wafanya biashara hao wameongeza kuwa gharama ya kutumia malori iko juu jambo ambalo linawafanya kupata hasara badala ya faida kwenye biashara zao.Hata Hivyo hivi sasa wamesema kuna matumaini baada ya serikali ua Uganda kuahidi kurekebisha reli kutoka mjini Kampala hadi Malaba na kuiunganisha na eneo hilo la viwanda ambalo ni zaidi ya ekari elfu 2. Serikali ya Kenya imesaini mkataba wa shilingi bilioni 116.2 bilioni na kampuni ya ujenzi ya Uhispania kukarabati reli ya kilomita 27 kutoka mjini Kampala hadi Namanve.