Taifa la Kenya liliagiza bidhaa zenye kima cha dola milioni 84 nchini Singapore
2021-08-17 07:56:14| cri

Taifa la Kenya liliagiza bidhaa zenye kima cha dola milioni 84 nchini Singapore, huku Kenya ikiuza bidhaa za kima cha dola milioni sita mwaka 2020 kwa mujibu wa data za Shirika la Fedha Ulimwenguni-IMF. Wakiwahutubia wanahabari kwa njia ya mtandao Msimamizi wa kampuni ya miundo mbinu ya Surbana Juronng ya Singapore katika eneo la Afrika Mashariki na Maghraibi Chike Uchendu amesema kuwa, Kenya ni moja ya mataifa yenye mazingira bora ya kufanyia biashara barani Afrika.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, biashara kati ya Singapore na Afrika imeongezeka kwa asilimia saba, huku taifa hilo likiwa miongoni mwa mataifa 10 yaliyowekeza Zaidi barani Afrika.

Baadhi ya sekta ambazo Singapore imewekeza barani Afrika ni pamoja na miundo msingi, teknlojia na mawasiliano, elimu, uchukuzi,afya na hoteli.

Singapore inaanda kongamano la siku mbili la biashara na mataifa ya Afrika, litakaloanza tarehe 23 hadi 24 mwezi huu.