Waziri ataka kutengwa maeneo uwekezaji
2021-08-30 08:03:32| CRI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wa Tanzania (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka wakuu   wa mikoa  na makatibu tawala nchini humo kutenga maeneo maalum, kwa ajili ya uwekezaji.

Alisema hayo katika ziara ya viongozi wa mikoa 26 katika mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kujifunza namna eneo hilo lilivyofanikiwa kutumia fedha za ndani katika miradi ya maendeleo na kutenga sehemu maalum kwa wawekezaji.

Wakuu hao wa mikoa pia walitembelea eneo la uwekezaji  wa viwanda vinane, lenye ukubwa wa ekari  600  na sehemu maalum, kwa ajili ya  wajasiriamali  yenye ukubwa wa ekari 500 katika wilaya ya Kahama.

Waziri Ummy alisema Manispaa ya Kahama, ambayo imeongoza  kwenye ukusanyaji mapato, ilipanga kukusanya Sh. bilioni 8.8, lakini ilivuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 9.6 sawa na asilimia  109.

Alisema manispaa hiyo ilipanga kupeleka Sh. bilioni 4.7  katika miradi ya maendeleo, lakini wamefanikiwa kupeleka Sh Bilioni 5.1