Marekani yajishushia hadhi kwa kutoa “Ripoti ya Biashara ya Magendo ya Watu”
2021-08-31 14:39:45| Cri

Marekani yajishushia hadhi kwa kutoa “Ripoti ya Biashara ya Magendo ya Watu”_fororder_VCG11392806450

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hivi karibuni ilitoa Ripoti yake ya mwaka 2021 ya Biashara ya Magendo ya Watu, na kwa mara nyingine tena, ilitumia mbinu yake ya kawaida ya kuweka vigezo viwili. Wakati inakosoa na kukashifu nchi nyingine ikiwemo China katika suala hilo, nchi hiyo inadai kwamba imefanya vizuri zaidi duniani katika kupambana na magendo ya watu.

Tarehe 23 Agosti ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa Duniani. Kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu ni “Kuondoa Tatizo la Ubaguzi wa Rangi kutokana na Biashara ya Watumwa kutoka Afrika: Jambo Muhimu zaidi la Kudumisha Haki Duniani”. Ripoti hiyo ya Marekani, ni nchi iliyonufaika zaidi na biashara ya watumwa wa Afrika ambao ni janga kubwa la kibinadamu katika historia, haijatafakari juu ya ongezeko la ubaguzi wa rangi na biashara ya magendo ya watu nchini humo, badala yake, inadai imefanya vizuri na kupaka matope nchi nyingine bila ya msingi wowote. Katika ripoti hiyo, Marekani imeorodhesha China kati ya nchi zenye hali mbaya zaidi ya magendo ya watu, na kuhusisha suala la Xinjiang na “biashara ya binadamu”, jambo linalowashangaza watu!

Kama tunavyojua, Marekani ilikuwa nchi iliyokua kufuatia “biashara ya watumwa kutoka Afrika”. Kulingana na rekodi iliyohifadhiwa kwenye jumba la makumbusho la rais wa awamu ya nne wa Marekani James Madison, mfumo wa utumwa ulikuwa injini kuu ya uchumi wa Marekani. Kuanzia mashamba ya pamba huko kusini, tumbaku katika kanda ya mashariki, hadi ujenzi wa meli huko kaskazini, sekta mbalimbali za Marekani zilitegemea mfumo wa utumwa. Mwaka 1850, asilimia 80 ya bidhaa zilizouzwa na Marekani kwa nchi za nje zilizalishwa na watumwa kutoka Afrika. Wakati huo, watumwa weusi walinyanyaswa kikatili na hata kuuawa na wamiliki wao wakati walipokuwa wakitengeneza utajiri kwa nchi ya Marekani. Walikuwa hawana haki zozote kama binadamu.

Hadi sasa Marekani bado haijabadilisha “mila yake ya kitaifa", na kuendelea na ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi na watu wa rangi nyingine. Takwimu zinaonesha kuwa, Wamarekani wenye asili ya Afrika wameathiriwa zaidi na janga la COVID-19. Kwa mfano, watu weusi wanachukua asilimia 30 mjini Chicago, lakini idadi ya watu weusi waliokufa kutokana na janga hilo ni asilimia 72. Waasia pia wamekumbwa na ubaguzi wa rangi wakati wa janga hilo. Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Utafiti la Pew la Marekani, asilimia 30 ya Wamarekani wenye asili ya Asia wamekushuhudia ubaguzi wa rangi.

Marekani ni moja ya nchi zenye tatizo zaidi la magendo ya binadamu. Mwaka 2004, Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani ilikiri hadharani kwamba, idadi ya watu waliosafirishwa kwenda nchi hiyo kutoka nchi nyingine kwa njia haramu ni kati ya 14,500 na 17,500 kila mwaka. Idadi hiyo imeongezeka zaidi katika miaka ya hivi karibuni nchini Marekani. Takwimu zinaonyesha kuwa, katika miaka mitano iliyopita, watu takriban 100,000 wanauzwa kwa nchi hiyo kila mwaka, na nusu yao wanalazimishwa kufanya kazi ngumu viwandani au wafanyakazi wa ndani majumbani. Profesa Laurel Fletcher kutoka Chuo Kikuu cha California amesema: “Watu wanaamini kwamba Marekani imekomesha mfumo wa utumwa, lakini kwa kweli, watumwa bado wapo, na mfumo wa utumwa umekuwa na sura mpya”.

Historia na hali ya sasa zinaonyesha kwamba, Marekani ni mhusika mkuu wa biashara ya magendo ya watu. Badala ya kulaani nchi nyingine, inapaswa kufanya vizuri mambo yake yenyewe, na kuondoa masuala ya ubaguzi wa rangi na magendo ya watu mapema zaidi.