Mwakilishi wa China UN atoa mwito wa mazungumzo na ushirikiano kutatua suala la silaha za kemikali la Syria
2021-09-03 09:03:11| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa mataifa Balozi Geng Shuang ametoa mwito wa kuwepo kwa mazungumzo na ushirikiano, pamoja na kurudi kwenye mkataba kuhusu silaha za kemikali, ili kutatua suala la silaha za kemikali la Syria.

Balozi Geng amesema ni muhimu kuendelea kuwepo kwa mazungumzo na ushirikiano kwenye kutatua suala hilo, na China inaitia moyo sekretarieti ya kiufundi ya Shirika la kupiga marufuku silaha za kemikali (OPCW) kuimarisha mazungumzo na Syria, ili kutatua kwa pamoja maswala yaliyobaki.

Bw. Geng pia ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mazungumzo na ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuheshimu ufuatiliaji halali wa Syria na kuepuka kutoa shinikizo la kisiasa.