Makundi yenye ushawishi ya Afrika yatoa mwito wa uwekezaji kwenye kilimo cha asili ili kupambana na njaa
2021-09-03 09:04:30| CRI

Makundi yenye ushawishi kuhusu mambo ya mazingira yametoa mwito wa kuwepo kwa uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kilimo kinachoweza kuhifadhi mifumo muhimu ya ikolojia ikiwa ni pamoja na maeneo ya vyanzo vya maji na misitu.

Makundi hayo yakiongozwa na kundi la Alliance for Food Sovereignty in Africa (AFSA) yameeleza umuhimu wa kilimo kilicho rafiki kwa mazingira ya asili, ili kuhakikisha usalama wa chakula na kuzoea mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa mjini Nairobi na mratibu mkuu wa AFSA Bw. Million Belay imesema wanakaribisha uwekezaji kwenye kilimo barani Afrika, lakini uwekezaji huo unatakiwa kuendana na matakwa ya wakulima wadogo wadogo, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuendana na mabadiliko ya tabia nchi, huku wakiendelea na kulinda afya ya viumbe wa maeneo yao.