Mtawala akiungwa mkono na watu wake, ataepuka kupoteza himaya yake
2021-09-06 14:18:07| CRI

Mtawala akiungwa mkono na watu wake, ataepuka kupoteza himaya yake_fororder_Hadithi za Jadi

Haya ni maneno ya busara ya wahenga wa China yakimaanisha ukiungwa mkono na watu, unaweza kuipata nchi, na ukipoteza uungaji mkono wao, basi utaipoteza nchi. Ni sawa na waswahili wanavyosema“Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe” au “Mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe”.