Tanzania yaweka vituo vingi zaidi kwa utoaji wa chanjo ya COVID-19
2021-09-13 09:25:42| cri

Tanzania yaweka vituo vingi zaidi kwa utoaji wa chanjo ya COVID-19_fororder_TZ

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amesema, Tanzania imeongeza vituo vya utoaji wa chanjo ya COVID-19 kutoka 550 hadi 1,548 ili kuwawezesha wananchi kuchanjwa.

Amesema ripoti za awali zimeonesha kuwa watu wengi zaidi wanakwenda kwenye vituo hivyo kuchanjwa.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alizindua kampeni ya utoaji wa chanjo ya COVID-19 mwezi Julai na kuwahakikishia watu wake kuwa chanjo hizo ni salama.

Bw. Misigwa amesema Shirika la Fedha Duniani IMF hivi karibuni liliidhinisha dola za kimarekani milioni 567.25 kusaidia juhudi za Tanzania za kukabiliana na janga la COVID-19 katika kushughulikia gharama za dharura ya kiafya, kibinadamu na kiuchumi.