Rais wa Afrika Kusini asema nchi yake yanufaika na jumuiya ya BRICS
2021-09-14 09:11:20| cri

Rais wa Afrika Kusini asema nchi yake yanufaika na jumuiya ya BRICS_fororder_VCG111124787035

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alisema Afrika Kusini imenufaika kwa kuwa mwanachama wa BRICS katika miaka kumi iliyopita, hasa kwenye sekta ya ushirikiano wa kiuchumi.

Amesema kujiunga na jumuiya hiyo ya uchumi kumeongeza nafasi ya Afrika Kusini ikiwa ni kundi jipya muhimu la uchumi duniani, hali ambayo inaweza kuipatia zaidi Afrika Kusini sera na utaalamu wa kiufundi, pia Afrika Kusini inaweza kupata uungaji mkono kutoka Benki ya Maendeleo ya nchi za BRICS.

Ameongeza kuwa uhusiano wa kibiashara unaendelea zaidi kati ya Afrika Kusini, China na India. Na kusisitiza kwamba kuanzishwa kwa Benki Mpya ya Maendeleo ya nchi za BRICS ambayo ina ofisi yake ya kikanda mjini Johannesburg, imekuwa ni muhimu katika kufadhili na kusaidia kiufundi miradi kwenye sekta za usafirishaji, nishati safi, uhifadhi wa mazingira, miundombinu ya maji, na kupunguza utoaji wa gesi chafu. Pia amesifu ushirikiano wa nchi za BRICS kwenye mapambano dhidi ya janga la Corona.