Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China yafafanua Mpango wa Utekelezaji wa Haki za Binadamu 2021-2025
2021-09-14 16:00:37| cri

 

Hivi karibuni serikali ya China imetoa Mpango wa Utekelezaji wa Haki za Binadamu wa Mwaka 2021-2025, uliotungwa kwa pamoja na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali na Wizara ya Mambo ya Nje, ambao umethibitisha malengo na majukumu ya kuheshimu, kulinda na kuhimiza haki za binadamu nchini China katika kipindi hiki.

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali leo imeitisha mkutano na wanahabari, ikifafanua maudhui makuu kwenye mpango huo.

Mpango huo unasema kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025, ni miaka mitano ya kwanza baada ya China kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora, kutimiza lengo la kwanza la Miaka Mia Moja na kuelekea lengo la pili la Miaka Mia Moja, na kufungua safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa.

Imefahamika kuwa mpango huo wenye sehemu nane unahusisha majukumu na malengo halisi 200.