Umoja wa Ulaya wasema hauna njia nyingine ila kuwasiliana na Taliban
2021-09-15 09:25:59| cri

Mkurugenzi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera ya mambo ya nje Bw. Josep Borrell amesema Umoja wa Ulaya hauna njia nyingine ila kuwasiliana na utawala wa Taliban nchini Afghanistan kama unataka kuishawishi nchi hiyo.

Akiongea kwenye mazungumzo ya kikao cha bunge la Ulaya kilichofanyika mjini Strasbourg nchini Ufaransa, Bw. Borrell amesisitiza kuwa mawasiliano kati ya Umoja wa Ulaya na Taliban hayamaanishi umoja huo unaitambua Taliban, bali ni kipaumbele kwa Umoja wa Ulaya kuendelea kuwalinda watu wengi kadri uwezekanavyo. Ameongeza kuwa kamati ya Umoja wa Ulaya imeongeza msaada wake mara nne, kutoka Euro milioni 50 hadi Euro milioni 200.

Umoja wa Ulaya unataka kuwasaidia wale wote wanaotaka kuondoka Afghanistan, ikiwa ni pamoja na watu wa nchi za Umoja wa Ulaya na watu wa Afghanistan waliopo hatarini.