Naibu balozi wa China katika UM atoa wito wa kufanyika juhudi za kuhimiza mchakato wa kisiasa nchini Sudan
2021-09-15 10:57:07| cri

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa balozi Dai Bing ametoa wito wa kufanyika juhudi za kuhimiza mchakato wa kisiasa nchini Sudan pamoja na maendeleo ya uchumi na ujenzi wa taifa.

Amesisitiza kuwa mchakato wa kisiasa nchini Sudan umepiga hatua nzuri kutokana na juhudi za pamoja za mamlaka za Sudan na wadau wengine, na kusema kuna haja ya kujenga kwa kasi na kuendelea kutoa msukumo kwenye mchakato wa amani na maendeleo ya Sudan.

Amefafanua kuwa serikali ya Sudan imefanya juhudi kubwa katika kutekeleza Makubaliano ya Amani ya Juba, ambapo China inapongeza muongozo wa kina wa makubaliano ya kisiasa uliopendekezwa na mamlaka za Sudan, ambao unafaa katika kupunguza wasiwasi kati ya pande mbalimbali na kuhimiza utekelezaji wa Makubaliano ya Amani ya Juba.