WHO yasema Afrika imetoa asilimia mbili tu ya chanjo ya UVIKO-19
2021-09-15 09:27:46| cri

WHO yasema Afrika imetoa asilimia mbili tu ya chanjo ya UVIKO-19_fororder_疫苗

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Afrika imeachwa nyuma na sehemu nyingine zote duniani kwani imepata asilimia mbili tu ya dozi zaidi ya bilioni 5.7 za chanjo ya UVIKO-19 zilizotolewa kote duniani, na kuionya dunia dhidi ya kutokuwepo kwa usawa katika utoaji wa chanjo.

Akiongea kwenye mkutano na wanahabari kupitia mtandao wa internet Dk Ghebreyesus amesema WHO inalenga kuchanja angalau asilimia 40 ya watu katika kila nchi hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu na asilimia 70 hadi katikati ya mwaka ujao. Hata hivyo ameeleza kuwa ni nchi mbili tu za Afrika zilizofikia lengo la asilimia 40, ambazo ni chache sana kuliko eneo lolote lile.

Mwaka jana WHO na washirika wake walizindua mpango wa COVAX ili kuhakikisha upatikanaji sawa na wa haki wa chanjo ya UVIKO-19, ambapo hadi sasa imetoa dozi zaidi ya milioni 260 kwa nchi 141.