Kenya yaitaka sekta binafsi kupiga jeki kampeni ya kuhifadhi wanyamapori
2021-09-15 10:56:15| cri

Kenya imeitaka sekta yake binafsi kupiga jeki kampeni ya kuhifadhi wanyamapori nchini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Utalii na Wanyama pori Najib Balala wakati akipokea fungu la pili la michango kutoka kwa wadhamini kupitia tamasha la Naming la Magical Kenya Tembo lililopangwa kufanyika Oktoba kwenye Mbuga ya Wanayama ya Amboseli ili kusaidia uhifadhi wa tembo, na kusema uhifadhi wa wanyamapori ni kazi inayotumia gharama kubwa ambayo haiwezi kutimizwa na rasilimali za umma pekee. Amesisitiza kuwa rasilimali za uhifadhi wa wanayamapori zinahitaji watu wawe wabunifu kwasababu sio rahisi, na hiyo ndio sababu ya kuanzisha kampeni ya kuchangisha pesa.

Kwa mujibu wa Balala hadi sasa tamasha la Naming la Magical Kenya Tembo limepokea jumla ya shilingi milioni 10 za Kenya na michango mingine inatarajiwa kupokelewa kabla ya tamasha hilo.