Nigeria yawakamata tena wafungwa 114 waliotoroka jela
2021-09-15 09:29:57| cri

Mamlaka nchini Nigeria zimethibitisha kuwa wafungwa 114 wamekamatwa tena baada ya kutoroka jela siku ya Jumapili jimboni Kogi, katikati ya nchi hiyo.

Kwenye taarifa yake, msemaji wa jela walikotoroka NCoS Francis Enobore alisema wafungwa hao waliokamatwa tena ni miongoni mwa wafungwa 240 waliotoroshwa kwa nguvu na genge la watu wenye silaha ambao walishambulia jela hiyo mjini Kabba, jimboni Kogi baada ya mapigano makali na walinzi.

Ameongeza kuwa hawatasita kuwasaka wafungwa wengine ambao bado wako mitaani.