Mwanadiplomasia wa China: Uingiliaji wa kijeshi ulioongozwa na Marekani wasababisha mgogoro wa kibinadamu nchini Afghanistan
2021-09-15 09:28:41| cri

Mwanadiplomasia wa China: Uingiliaji wa kijeshi ulioongozwa na Marekani wasababisha mgogoro wa kibinadamu nchini Afghanistan_fororder_阿富汗

Balozi wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Jiang Duan amesema, uingiliaji wa kijeshi ulioongozwa na Marekani ni sababu kuu ya mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

Balozi Jiang ameeleza wasiwasi mkubwa juu ya hali ya Afghanistan kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa niaba ya kundi la nchi zinazoshiriki katika Kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo imesema hadi kufikia mwezi Aprili mwaka 2020, takriban watu 47,000 wa Afghanistan waliuawa katika vita vilivyofanywa na Marekani na waafghanistan zaidi ya milioni 10 walipoteza makazi yao. Nchi jirani pia zimeathiriwa vibaya na uingiliaji wa kijeshi ulioongozwa na Marekani.

Taarifa hiyo inamtaka kamishna mkuu wa Haki za Binadamu kuendelea kufuatilia madhara yanayotokana na uingiliaji wa kijeshi wa nchi zinazohusika juu ya haki za binadamu za waafghanistan, na kuziwajibisha nchi hizo kwa uhalifu wa wanajeshi wao wa kuwaua watu wa Afghanistan.