WHO yasema huenda Afrika isifikie lengo la kuchanja asilimia 40 ya watu kutokana na upungufu wa chanjo
2021-09-17 10:23:49| cri

WHO yasema huenda Afrika isifikie lengo la kuchanja asilimia 40 ya watu kutokana na upungufu wa chanjo_fororder_VCG111341244696

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO kanda ya Afrika Bw. Matshidiso Moeti amesema kuwa lengo la kuchanja asilimia 40 ya watu wa Afrika dhidi ya COVID-19 ifikapo mwezi Disemba linaonekana kuwa gumu kutimia wakati bara hilo likikabiliwa na uhaba wa usambazaji wa dozi kupitia majukwaa mbalimbali.

Ameongeza kuwa bara hilo linakabiliwa na upungufu wa chanjo milioni 500, wakati kituo cha COVAX kinapunguza dozi milioni 150 ambazo zilipangwa kutolewa mwaka huu.

Bw. Moeti amesema kuwa kituo cha COVAX kitatoa dozi milioni 470 tu za chanjo kwa Afrika mwaka huu, ambazo zinatosha kuchanja asilimia 17 ya watu, na kuongeza idadi ya watu waliopewa chanjo kamili.